Jumamosi, 15 Novemba 2014

PICHA RASMI KUTOKA IKULU:JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMED CHANDE OTHMAN AMJULIA HALI RAIS JAKAYA KIKWETE NCHINI MAREKANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo
ya mahakama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga.

About the Author

Ukurasa wetu

Author & Editor

Has laoreet percipitur ad. Vide interesset in mei, no his legimus verterem. Et nostrum imperdiet appellantur usu, mnesarchum referrentur id vim.

Chapisha Maoni

 
Ukurasa wetu © 2015 - Mark Mugan| Designed and Developed by Mark Mugan | call +255 673 111 069