Alhamisi, 13 Machi 2014

Kura 487 zampa Sitta Uenyekiti Bunge Maalum la Katiba

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wasira akiwa na Mjumbe mwenziwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura ya nafasi ya Mwenyekiti leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na mjumbe wa bunge Sadifa Sadifa, wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura ya nafasi Mwenyekiti leo, Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombea katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Hashim Rungwe akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombea katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa akiweka karatasi ya Kura yake ya Kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakipigakura kwa ajili ya nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, iliyokuwa ikiwaniwa na Bw. Samuel Sitta na Bw. Hashim Rungwe leo, Mjini Dodoma.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa na Anna Tibaijuka wakimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Bunge maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta Mara baada ya Kutangazwa Kuwa Mshindi wa Nafasi hiyo kwa Idadi ya Kura 487 dhidi ya Hashim Rungwe aliyepata kura 69 na kura zilizoharibika  ni 7.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombea katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka wakati zoezi la upigaji kura likiendelea leo Mjini Dodoma. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)

About the Author

Ukurasa wetu

Author & Editor

Has laoreet percipitur ad. Vide interesset in mei, no his legimus verterem. Et nostrum imperdiet appellantur usu, mnesarchum referrentur id vim.

Chapisha Maoni

 
Ukurasa wetu © 2015 - Mark Mugan| Designed and Developed by Mark Mugan | call +255 673 111 069